BABA WA DIAMOND PLATINUMS AKATALIWA KUMUONA MJUKUU WAKE TIFFAH
Baba mzazi wa mwanamuziki huyo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Jumaa ‘Baba D’.
MSHTUKO! Baada ya hivi karibuni staa
wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kupata mtoto wa kike,
Latifah Nasibu ‘Princes Tiffah’ kupitia kwa mwandani wake, Zarinah
Hassan ‘Zari The Boss Lady’, baba mzazi wa mwanamuziki huyo, Abdul Jumaa
‘Baba D’ amekataliwa kumuona mjukuu wake huyo, Risasi Mchanganyiko lina
habari kamili.
Kwa mujibu wa baba Diamond, baada ya
Tiffah kuzaliwa Agosti 6, mwaka huu, mama mzazi wa nyota huyo, Sanura
Kassim a.k.a Sandra alimpigia simu mzazi mwenzake huyo na kumjuza kwamba
wamepata mjukuu, jambo ambalo walilifurahia kwa pamoja.
0 comments Blogger 0 Facebook
Post a Comment