Kama kuna ajali ambazo zimewahi kunishtua ni hii hapa, kwanza najiuliza dereva hakuona au ilikuwaje mpaka hii basi ikanasa hapa!
Ndani ya Basi kulikuwa na Wanafunzi 60
wa Kihispania, wametoka zao Bilbao kwenda Amsterdam bahati mbaya hii
ajali ikatokea wakiwa eneo la La Madeleine, Ufaransa…
Mwanafunzi mmoja amesema wengi wao walikuwa wamelala ndani ya basi,
wakashtukia tu gari imenasa chini ya daraja na imekatika sehemu yote ya
juu.
Majeruhi wengi walikuwa waliokaa kwenye
siti ya nyuma, walipelekwa Hospitali na wengine ilibidi waahirishe tour
yao na kurudi nyumbani kwao Hispania.
Dereva alikamatwa na kupimwa wakakuta
hakuwa amelewa wala hakuwa na tatizo lolote, alichojitetea ni kwamba
alikuwa akifata maelekezo ya barabara kwa kutumia GPS na hakuwa
amegundua kwamba daraja hilo lina urefu ambao basi lake haliwezi kupita
!!
Hii video ni ajali ya aina hiyohiyo iliyotokea Uingereza 2013, basi likakatika baada ya kupita chini ya daraja la treni.
0 comments Blogger 0 Facebook
Post a Comment