Breaking news zilizoifikia
saa nne usiku wa July 30 2015 kutoka Baraza la sanaa Tanzania (BASATA)
ni kwamba baraza hili limemfungia Shilole kutojihusisha na kazi yoyote
ya sanaa kwa muda wa mwaka mmoja.
Barua iliyoifikia, ambayo imeandikwa kutoka BASATA imesema >>> ‘Tarehe
9 May 2015 ukiwa katika onyesho lako la muziki Ubelgiji ulicheza uchi
mbele ya hadhira ya wapenda sanaa za Tanzania hivyo kudhalilisha utu
wako na jamii ya kitanzania kimaadili‘
‘BASATA
ilipata habari zako, kumbuka pia October 2013 BASATA lilikuonya na
ukakiri kwa kuomba msamaha tabia yako ya kucheza bila kuzingatia maadili
uwapo jukwaani, BASATA ilikupa nafasi ya kutoa maelezo kwanini
usichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo chako lakini umekaidi kutoa
maelezo yako‘ – BASATA
‘Baraza
limejiridhisha kwamba ulikiuka maadili ya kazi ya sanaa kwenye onyesho
lako huko Ubelgiji makusudi na umekiuka sheria kwenye ibara ya 30 (2) ya
katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa kuvunja
maadili ya jamii ya Mtanzania hivyo baraza linakusimamisha
kujishughulisha na kazi za sanaa nchini na nje ya nchi kwa mwaka mmoja,
kufanya kinyume na hayo kutapelekea kupewa adhabu zaidi pamoja na yeyote
utakaeshirikiana nae ‘ – BASATA
Home
»
» Unlabelled
» BASATA IMEMFUNGIA SHILOLE MWAKA MMOJA, HAKUNA KUFANYA MUZIKI, SABABU HIZI HAPA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments Blogger 0 Facebook
Post a Comment